Maonesho ya nanenane 2024 kanda ya ziwa magharibi yamezinduliwa rasmi leo Agost 3,2024 kwenye viwanja vya Nyamhongolo huku yakionesha kuzidi kupata hamasa kutoka kwa wananchi.
Akifungua maonesho hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Katibu Tawala wa Mkoa huo Ndugu Mohamed Gombati amesema jukwaa hilo liendelee kuwa somo kwa makundi mbalimbali yanayolengwa na maonesho hayo.
Akiwa na mwenyeji wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndugu Balandya Elikana, Gombati ametembelea mabanda mbalimbali na kujionea huduma zitolewazo na taasisi,Halmashauri na makundi mbalimbali.
"Serikali ya Rais Samia inataka Taifa lijitosheleze kwa chakula, uwekezaji katika kilimo na maendeleo ya viwanda,nimeona fulsa hizo hapa nanenane" amesema Gombati
Akitoa taarifa ya maonesho hayo Ndugu Balandya amebainisha kuwa maonesho hayo yamekuwa na tija kwa wajasiliamali kutokana na kupata elimu ya utalaamu wa kuendesha shughuli za kilimo.
" eneo letu idadi kubwa ni wakulima, wafugaji na wavuvi, Serikali inaendelea kuwekeza katika sekta hii hivyo wakulima wanafaidika kwa kufanya shughuli zao kwa tija" a.esema Balandya
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.