Prof.Faustin Kamuzora Katibu tawala wa Mkoa wa Kagera mgeni rasmi wa leo tarehe 07/08/2020 kwenye maonyesho ya nanenane Mkoa wa Mwanza,ametembelea mabanda ya maonyesho ya Kwimba hapo amepata elimu ya kilimo cha mazao mbalimbali yakiwemo mazao ya malisho ya mifugo,kilimo cha Pamba,Mpunga,Dengu,Choroko,Mhogo,Uwele, Alizet,matunda ya papai,Tikiti maji na Tango.
Aidha Prof. Kamuzora amepata elimu ya ufugaji wa mbuzi wa maziwa hapo akataka kujua kiasi Cha maziwa kinachozalishwa kwa siku, Ndug. Jems Mnyeti Mfugaji wa mbuzi wa maziwa akaelezea kuwa mbuzi hao wanauwezo wa kutoa Lita tatu za maziwa kwa siku kama wanapata chakula chakutosha.
Prof. Kamuzora ametaka kujua kama kuna wananchi wa Wilaya ya Kwimba wanaojishughulisha na kilimo cha malisho ya mifugo kama chanzo cha mapato na ameshauri wananchi waichukue hii kama fursa ya kuwaingizia kipato kwani wananchi wanaweza kulima na kuuza malisho ya mifugo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.