Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandis Robert Gabriel awataka wasimamizi wa ujenzi wa madarasa kuhakikisha wanajaza fomu za usimamizi wa vifaa vya ujenzi ili kudhibiti upotevu wa vifaa.
Mhandisi Gabriel ameyasema hayo leo tarehe 29/11/2021 wakati akifanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya miradi ya ujenzi wa madarasa katika Shule za Sekondari. Miradi inayotekelezwa kwa fedha za UVIKO-19 ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ilipokea Bilion 2.18 kwaajili ya ujenzi wa madarasa 109.
Akiongea katika ziara hiyo Mkuu huyo amesema fomu hizo zinapaswa kujazwa kila siku ili kuonyesha vifaa vinavyokuwa vimetumika katika ujenzi kwa siku husika.
Aidha Mhandisi ameupongeza uongozi waHalmashauri ya Wilaya ya Kwimba kwa hatua iliyofikiwa ya ujenzi na kwakuona umuhimu wa kununua vifaa vyote vya ujenzi kwa pamoja ili kupunguza gharama na kuokoa kiasi cha fedha ambacho kitaweza kutumika katika shughuli nyingine.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa akishirikiana na viongozi wa Wilaya akiwemo Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wameshiriki shughuli za ujenzi ikiwemo kusogeza tofari na kuchanganya zege katika Shule za Igongwa, Ngudu na Maligisu.
Ziara hiyo imehusisha ukaguzi wa ujenzi wa Madarasa katika Shule za Igongwa, Ngudu, Walla, Iseni na Maligisu ambapo pamoja na kupongeza, wameshauri kasi iongezwe zaidi na usimamizi uendelee kuimarishwa.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.