Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mheshimiwa Amos Makalla amewataka watumishi wa umma kutoa huduma bora Kwa wananchi wanaofika katika maeneo yao ya kazi kwaajili ya kupata huduma.
Ameyasema hayo leo Juni 2,2023 wakati akijitambulisha kwa viongozi na watumishi wa Wilaya ya Kwimba " nimefurahi kufika Kwimba na nimekuja kuwakumbusha kuwa tupende kazi zetu,watumishi wa Serikali tutoe huduma bora, tuwe wasikivu, tuwe na nidhamu na tufanye kazi" amesema Makala
Mkuu huyo amesisitiza nidhamu ya kazi na kufanya kazi kwa bidii Ili kujiongezea kipato na kupata mafanikio ambayo ni hitaji la Kila mwananchi " fanyeni kazi hakuna mafanikio yanayokuja kama miujiza kama baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa jadi wanavyosema haipo, njia peke ya kupata mafanikio ni kufanya kazi" Makala
Aidha Mheshimiwa Makala ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kwa kutoa fedha za mapato ya ndani zaidi ya 40% kwaajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo. Pia amesisitiza ulinzi wa vifaa vinavyotumika kutekeleza miradi ya maendeleo ' tukiruhusu wizi wa vifaa tunajiibia wenyewe' tuimarishe ulinzi ili miradi yote ikamilike kwa wakati.
Mheshimiwa Makala ameahidi kutoa ushirikiano kwa wananchi wote na viongozi wa Wilaya ya Kwimba ili kutoa huduma na kufikia maendeleo ambayo ndio shauku ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
Viongozi walioshiriki kikao hicho wameahidi kwenda kufanyia kazi maelekezo aliyotoa Mkuu wa Mkoa " tunakuahidi kwenda kufanya kazi, kuhudumia wananchi, na pale penye tatizo tutalitatua ili tuwafikie wananchi kama inavyotakiwa" amesema Mhe. Thereza Lusanga Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.