Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kuwa wabunifu kwenye ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kuweza kuongeza mapato na bajeti.
Amesema hayo leo (Januari 15, 2023) wakati wa kikao kazi cha pamoja na Halmashauri ya Kwimba kilichojadili kuhusu vigezo muhimu vya kuzingatia katika maandalizi ya bajeti ya mwaka 2023/24.
Malima amesema uhai wa Halmashauri yoyote hutegemea sana makusanyo ili kukidhi Utekelezaji wa shughuli za kila siku kupitia bajeti zilizopangwa na kwa mujibu wa sheria hivyo wanapaswa kuwa na mpango wa kukusanya mapato mengi zaidi.
“Kwa jinsi nilivyowasikiliza nimebaini mna vyanzo vizuri sana vya mapato na mnaweza kukusanya zaidi hata ya Bilioni Tano na wala sio kama mlivyokadiria wenyewe kufikia kwenye Bilioni 3.1 tu na bora mngekadiria fedha nyingi ili mjitume zaidi” Malima.
Naye, Katibu Tawala Mkoa Balandya Elikana ameitaka Halmashauri kuhakikisha inatenga bajeti ya mapato ya ndani kwaajili ya kununua taulo za kike za wanafunzi wa shule za sekondari wale wasio na uwezo wa kununua taulo hizo
“madiwani simamieni hili bajeti ijayo mpange kuwanunulia taulo watoto wa kike ambao wazazi wao hawana uwezo wa kuwanunulia watoto wao, msisubiri fedha za Serikali kuu tu wekeni bajeti kwenye mapato ya ndani” amesema Balandya
Akitoa taarifa ya Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji Bi.Happiness Msanga amefafanua kuwa kwa mwaka 2023/24 Halmashauri imekadiria kukusanya zaidi ya Bilioni 3 wakati kwa mwaka wa fedha unaoendelea
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.