Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA. Amos Makala amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Kwimba na uongozi wa Halmashauri ya Kwimba kuhakikisha wanasimamia na kutoa elimu kwa wazazi na jamii kwa ujumla juu ya umuhimu wa elimu kwa watoto ili kutokomeza suala la utoro na kukuza ufaulu shuleni.
"Swala la utoro shuleni, ufaulu na watu kutokumaliza shule niwaombe sana watendaji wetu tutoe elimu hiyo ya umuhimu wa watoto wetu kusoma na kuhakikisha ni ajenda yetu sote na sio afisa elimu tu na jamii nzima ielewe umuhimu wa kuwapeleka watoto shule kwa kuwa Serikali ya awamu ya sita imeboresha miundombinu ya elimu hakuna sababu ya watoto kutokwenda shule," amesema Makalla.
Mhe.Makalla amesema hayo leo Juni 27, 2023 kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kwa ajili ya kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) za Mwaka 2021/22.
Aidha Mkuu huyo amewataka viongozi wa Wiaya ya Kwimba kutafuta suluhu katika Ukusanyaji wa ushuru kwa wafanyabiashara waliojenga vibanda katika stendi ya Ngudu na Malya.
"Niwaombe mkae nao muwaeleze kwamba eneo lile ni la serikali na wanachotakiwa kufanya na mkuu wa wilaya uongoze kikao hicho, muwabaini wachochezi wa mgogoro ambao hawahusiki na eneo hilo mkae katika majadiliano na watu wanaohusika na vile vibanda, mpate orodha ya watu waliokubali kusaini mikataba na kulipa na mpate orodha ya watu waliogoma kulipa," RC Makalla.
Vilevile, Mhe. Makalla ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kwa kupata Hati Safi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na amewataka Madiwani kufanyia kazi na kuijadili taarifa ya mkaguzi mara kwa mara.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija amemuahidi Mkuu wa Mkoa kwa niaba ya watumishi, kamati ya usalama na Kwimba kwa ujumla kwamba watasimamia maelekezo yote aliyoyatoa.
Halikadharika, Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Mkoa wa Mwanza Waziri Shabani kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amesema Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imepata hati safi inayoridhisha kutokana na ushirikiano alioupata kwa watumishi wa Halmashauri hiyo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.