Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Juni 06, 2024 amezungumza na watumishi wa Halmashauri wa Wilaya ya Kwimba na akatumia wasaa huo kutoa dira ya kuwaletea wananchi maendeleo kupitia majuk doumu yao kuwa ni uzingatiaji wa nidhamu katika kazi.
Akizungumza na watumishi hao kwenye Ukumbi wa Halmashauri, Mtanda amewataka watumishi hao kuacha kuishi kwa mazoea na badala yake wawe na nidhamu ya kuwahi kazini na kujituma ili kuhakikisha wanawatumikia wananchi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za miongozo.
Aidha, amewataka watumishi kujenga umoja baina ya taasisi moja na nyingine ndani ya wilaya na kushirikiana kwenye kazi na kuepuka tabia ya ubishani au makundi kazini ili kila mmoja ajue ana wajibu wa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na sio kwa ajili ya mtu fulani na vinginevyo.
Vilevile, amewapongeza kwa ukusanyaji wa Mapato hadi kufikisha shilingi Bilioni 3.5 kutoka Bilioni 2 za siku za nyuma na amewakumbusha kutumia fedha kwa mujibu wa Miongozo iliyopo kwa kutenga 10% za Makundi ya kisheria, 40% za miradi ya maendeleo na kuwahimiza wakusanya mapato kuweka fedha benki.
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija amesema kuwa upatikanaji wa Maji vijijini kwa sasa ni asilimia 62 na ipo miradi kadhaa ya maji inaendelea kutekelezwa na kwamba itakapokamilika itasaidia wilaya hiyo kufikia asilimia zaidi ya 70 ya upatikanaji maji safi.
Aidha, amebainisha uwepo wa nishati ya umeme kwenye vijiji vyote wilayani huku akifafanua kuwa ukusanyaji wa mapato kupitia TRA wamekusanya zaidi ya Bilioni 2 tofauti na Bilioni 1 waliyoikusanya mwaka uliopita ikiwa ni ongezeko linalotokana na sera nzuri za serikali ya awamu ya sita.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.