Mgeni rasmi Ndug.Nyakia Ally Katibu tawala wilaya akihutubia katika mahafali ya kidato cha nne Shule ya Sekondari Bupamwa tarehe 09/10/2020 amesema pamoja na shule kupokea milioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa hosteli bado shule inauhitaji wa hosteli nyingine kwani wanafunzi ni wengi na wanatembea umbali mrefu kufika shuleni.Vilevile amewashauri wazazi wa wanafunzi kuongeza ushirikiano na shule ili kuwasaidia wanafunzi kufanya vizuri kwani wazazi wameaswa kutowaozesha wanafunzi wa kike kwa lengo la kijipatia Ng'ombe na fedha,kwani katika shule hiyo kuna Mwanafunzi aliyekimbia nyumbani kwao kwasababu wazazi wake walitaka aache masomo ili aolewe.Pia amesema wanafunzi ambao ni watoro watakamatwa wazazi wao ili wazazi waone umuhimu wa kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Bupamwa Mwalim Helman Daudi Shingisha akisoma risala ya shule kwenye mahafali hiyo amesema shule inapata changamoto ya wanafunzi kuacha shule na wengine kuwa watoro wa lejaleja kutokana na wazazi kutowahamasisha wanafunzi kupenda masomo, umbali mrefu kutoka nyumbani hadi shuleni na sababu nyingine za kibinafsi.Mkuu huyo ameorodhesha changamoto za shule hiyo ikiwemo nyumba za walimu kutokuwa na umeme,kukosekana kwa mashine ya kurudufu (photocopy machine) ambapo wageni waliohudhuria mahafali hayo wameweza kuchangia fedha zaidi ya milioni tatu na mwingine ameahidi kuwaletea mashine ya kurudufu ifikapo mwezi wa 12.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Bupamwa wameishukuru serikali kwa kuleta fedha za kujenga hosteli lakini wameiomba serikali kuongeza hosteli nyingine ili wanafunzi wote waweze kuishi shuleni waepukane na adha ya kutembea umbali mrefu ( kilomita 32 kwenda na kurudi) hali inayowapelekea kufika shuleni wakiwa wamechoka na hivyo kutojisomea vizuri
Mgeni rasmi Ndug.Nyakia akikabidhi vyeti kwa wahitimu
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.