Wakazi wa kata ya Ngudu Wilayani Kwimba leo tarehe 22/08/2022 wameshiriki katika uchumbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa bweni la watoto wenye ulemavu (viziwi, vipofu, wenye ulemavu wa viungo na albino) katika Shule Ya Msingi Kakora iliyopo ngudu. Halmashauri Ya Wilaya Ya Kwimba inajumla ya wanafuzi wenye ulemavu mia tano sabini (570) huku Shule ya msingi kakora ikiwa na watoto wenye ulemavu tisini na nne (94).
Afisa elimu wa elimu maalum wilaya ya kwimba Mwalimu Faraja Isaya Chubwa amesema kuwa Halmashauri imepokea kiasi cha shilingi milioni mia moja (100) kwaajili ya ujenzi wa bweni la watoto wenye ulemavu katika shule ya msingi kakora, kiasi hicho cha fedha kitasaidia katika kukamilisha ujenzi wa jengo na miundo mbinu yamaji safi na maji taka ya bweni hilo.
Aidha Afisa huyo amesema bado kuna uhitaji mkubwa wa mabweni ya wanafunzi wenye uhitaji maalumu kwani wanafunzi wengi wanashindwa kuhudhuria Shuleni kutokana na umbali kutoka nyumbani hadi Shuleni. Amesisituza kuwa ujenzi wa bweni hilo utasaidia wanafunzi wengi wenye mahitaji maalumu kupata Elimu.
Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kakora Faida Daniel amesema anayo furaha kubwa kupokea mradi huo wa ujenzi wa Bweni kwa ajili ya watoto wenye ulemavu katika shule yake kwani anaamini kabisa mradi huo utasaidia kuongeza hali ya ufaulu kwa wanafuzi wenye ulemavu. Lakini pia ameiomba Serikali kaujili walimu wenye taaluma ya kufundisha watoto wenye ulemavu kwani walimu waliopo sasa wengi hawana taaluma ya kufundisha watoto hao kitu kinachopelekea kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi hao.” Niiombe Serikali iendelee kuajili walimu wa wanafunzi wenye ulemavu ili kurahisisha kazi ya ufundishaji kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu” amesema Faida Daniel
Wananchi nao wametoa maoni yao juu ya mradi huo wa ujenzi wa bweni hilo. John Mwibonya Lwambo mkazi wa Ngudu amesema kuwa serikali imefanya kitu bora sana kwani itasaidia kwa kiasi kikubwa sana katika ufaulu wa wanafunzi hao hivyo ameiomba Serikali kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya Wilaya ya Kwimba.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.