Shule ya Sekondari Nyamilama imepongezwa kwa kuongoza ufaulu kidato cha pili na cha nne kwa matokeo ya mwaka 2022.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga aliyekuwa mgeni rasmi katika sherehe za mahafali ya 17 ya kidato cha nne iliyofanyika leo Oktoba 20,2023 katika Shule hiyo
" niwapongeze Walimu, wanafunzi na wazazi kwa ushirikiano mnaoufanya katika kuhakikisha Shule hii inakuwa na matokeo mazuri Kitaifa,endeleeni na juhudi hizo Ili mwaka huu matokeo yawe mazuri zaidi"
Aidha Mkurugenzi amewataka wanafunzi wa kidato cha nne kuendelea kujiandaa na mitihani, pia amewashauri watakapomaliza mitihani wakajiunge na kozi za muda mfupi Ili waendelee kusoma pindi watakapokuwa wanasubiri matokeo
Shule hiyo imekuwa ikiongoza katika matokeo ya kidato cha pili na nne ambapo mwaka 2022 Katika matokeo ya kidato cha nne Shule hiyo ilikuwa ya kwanza kiwilaya na ilikuwa ya pili kimkoa.
Akisoma Risala ya Shule Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Johannes Katunzi amesema watumishi wa Shule hiyo wanafanya kazi kwa ushirikiano ndiyo maana matokeo ni mazuri, pia ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mama shupavu Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi za miradi ya maendeleo ambapo kwa mwaka 2023 madarasa 12 yamejengwa, bweni moja na maabara.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.