Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, ambayo huazimishwa tarehe 3 Machi kila mwaka, Wanawake wa Wilaya ya Kwimba wamesherehekea kwa kushiriki michezo mbalimbali ikiwemo kukimbiza kuku, kukimbia kwenye gunia, kuvuta kamba na michezo mingine.
Mheshimiwa Johari Samizi Mkuu wa Wilaya ya Kwimba ambaye alikuwa Mgeni rasmi wa sherehe hiyo Akiongea na wanawake hao amewaasa kufanya kazi kwa bidii ili kuchagiza maendeleo ya Wilaya na Taifa kwa ujumla. Mkuu huyo amewasisitiza Wanawake kutosahau wajibu wao kama wazazi na walezi wa familia hivyo pamewaasa kufanya kazi za kiuchumi kwa bidii na kutunza familia inavyotakiwa ili kutengeneza kizazi bora cha badae.
Akielezea kauli mbiu ya Siku ya Wanawake iliyokuwa ikisema " Kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu, Tujitokeze kuhesabiwa" amesema maendeleo endelevu hayawezi kuja kama wanawake wote hatutafanya kazi kwa bidii na kutoa malezi bora kwa watoto wetu, vilevile amesisitiza Wananchi kuwa tayari kuhesabiwa pindi kazi ya sensa itakapoanza.
Mheshimiwa Samizi amewataka wanafunzi wa kike kusoma kwa bidii na kujiepusha na vishawishi vinavyoweza kusababisha ndoto zao kutofikiwa
" jiepusheni na mafataki, wakiwafata kataeni tena wambieni kama wanapenda yunifomu wakawashonee wake zao, sisi hapa tungekatizwa ndoto zetu msingetuona hapa, kuweni na msimamo ili mfikie ndoto zenu" amesema Samizi
Naye Katibu wa CCM Ndugu Latifa Malim amewashauri wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama pindi mchakato wa uchaguzi utakapoanza.
Bi Happiness Msanga Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba amewashukuru Wanawake wote walioshiriki maadhimisho hayo na amewapongeza wajasiliamari waliofika na bidhaa zao ili kuonyesha na kuuza vitu wanavyovitengeneza
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.