Kamanda wa Police Wilayani Kwimba SP Mayombo Mtaju amelitaka jeshi la Sungusungu kuacha kujichukulia Sheria mkononi badala yake wafanye kazi za kulinda wananchi na Mali zao maana ndilo jukumi lao kubwa, pamoja na kukamata wahalifu siyo kuwapa adhabu ya vipigo,faini na kuwatenga.
Ameyasema hayo leo Machi 1,2023 wakati akiwapa Elimu ya ukamataji salama wa wahalifu " nyie ni wasaidizi wa polisi na kwasababu mnatusaidia sisi hamtakiwi kutoa adhabu Kwa wahalifu kazi yenu ni kuwakamata na kuwapeleka kwa mlinzi wa amani( Mtendaji wa Kijiji au Kata) au mnawapeleka kituo cha police Ili hatua za kisheria zifuatwe, kazi ya kutoa adhabu niyamahakama siyo jeshi la Sungusungu" amesema Mtaju
Aidha Afande Mtaju amelitaka jeshi la Sungusungu kutoa ushirikiano katika kufichua wahalifu hasa wauaji kama wanavyotoa ushirikiano kufichua wezi wa mifugo
" niwaombe mtoe ushirikiano kufichua wauaji, inasikitisha kwamba ng'ombe wakiibiwa mnamtafuta mwizi hadi mnmpata lakini mauaji yakitokea hakuna anayejitokeza kutoa taarifa hii siyo sawa, watajeni wahalifu wote Ili tutokomeze uhalifu"
Naye Mtemi wa Sungusungu Mogani Shimbi amewashauri Sungusungu kuzingatia maelekezo yote yaliyofundishwa na kamanda Ili waweze kufanya kazi zao Kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizowekwa na Serikali.
Katika mafunzo hayo yameshiriki majeshi tisa ya Sungusungu kutoka Kata ya Mwakilyambiti ambao wamemshukuru Afande Kwa mafunzo hayo, na wameshauri mafunzo hayo yatolewe marakwamara Ili yawasaidie kuacha kufanyakazi kwa mazoea.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.