Katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo Kiwilaya yamefanyika Ngudu Kwimba Mgeni Rasmi Mhe.Senyi S.Ngaga Mkuu wa Wilaya ya Kwimba amewashauri Wanawake kufanya kazi kwa bidii,kila mwanamke ambaye anasimamia kazi yoyote ile aifanye kwa weredi wa hali ya juu ili kuwe na maendeleo makubwa yanayotokana na mchango wa Wanawake kama viongozi.
Aidha Mhe.Ngaga amesema Wilaya ya Kwimba inao viongozi wengi Wanawake kuanzia yeye mwenyewe, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Mwenyekiti wa Halmashauri, baadhi ya Wakuu wa Idara kama Maji,Kilimo, Maendeleo ya Jamii na viongozi wengine hivyo ameshauri watumishi wote kila mmoja kwa sehemu yake kufanya kazi zitakazo chagiza maendeleo ya Wilaya ya Kwimba.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ya mwaka 2021 yamebeba kauli mbiu isemayo "Wanawake katika Uongozi chachu kufikia Dunia yenye Usawa" Kupitia kauli mbiu hii viongozi waliohudhuria Sherehe hiyo wamewaasa Wanawake wote kufanya kazi kwani zama za Mwanamke kujifutika ndani zilishapitwa na wakati sasa ni kazi tu.
Katika Maadhimisho haya Wanawake wajasiliamali wa Kwimba wameweza kuonyesha bidhaa mbalimbali wanazozitengeneza ili kujiongezea kipato, baadhi ya bidhaa hizo ni Chaki,Sabuni,Batiki,Nyungu kwa ajili ya kujifukiza,Mikoba,Mapambo na vingine vingi.Pia kupitia Risala yao wameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwapatia mikopo inayowawezesha kuendeleza miradi midogomidogo wanayoianzisha.
Katika maadhimisho hayo wamehudhuria wanafunzi wa kike ambao wameaswa kusoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zao na kutengeneza Mazingira ya kuwa viongozi wakubwa wa badae.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.