Wizara ya Afya maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto wakishirikiana na Mkoa wa Mwanza na Idara ya Afya Wilayani Kwimba wamefanya ukaguzi katika Taasisi mbalimbali kuangalia hatua zinazoendelea kuchukuliwa za kujikinga na virusi vya corona na kuwahamasisha watu wote kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa COVID_19.
Katika zoezi hilo shule mbalimbali za Msingi na sekondari zimetembelewa ikiwemo shule ya sekondari Ngudu,Bujiku Sakila na Malya katika shule hizo tahadhari zimeendelea kuchukuliwa kwa kuweka maji ya kunawa maeneo mbalimbali,wanafunzi kukaa mbalimbali madarasani na elimu kwa wanafunzi inaendelea kutolewa.
Aidha Idara hiyo imefika katika vyuo vilivyopo hapa Kwimba ambavyo ni Chuo cha michezo Malya na Chuo cha maendeleo ya wananchi Malya hapo tahadhari zinaendelea kuchukuliwa kwani wanafunzi wametawanywa katika mabweni ya kulala ili kupunguza msongamano wengine wanalala kwenye madarasa,maji ya kunawa yamewekwa maeneo mbalimbali,elimu inatolewa marakwamara na tahadhari nyingine zinazingatiwa.
Watalaamu hao wa Afya wamepita katika mikusanyiko ya watu (minadani) na kutoa elimu kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa COVID-19.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.