Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU yakabidhi Milioni sita kwa Mkuu wa Wilaya Kwimba.
Kamanda wa TAKUKURU Kwimba Ndug. Julian Augustine amekabidhi kiasi cha Milioni sita kwa Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe.Senyi Simon Ngaga.Zoezi hilo la makabidhiano ya fedha limefanyika Ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Kwimba leo tarehe 21/01/2021, mbele ya kamati ya ulinzi na usalama.
Akiongea kabla ya kukabidhi fedha hizo kamanda huyo amesema fedha hizo zimetokana na ufuatiliaji wa kazi ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kadashi ambapo Fundi mmoja alitoroka na kukimbia na fedha ya Serikali kabla ya kukamilisha mkataba. Fundi huyo alikamatwa na amerudisha fedha yote ambayo hakuifanyia kazi.
Baada ya mapokezi ya fedha hizo Mkuu wa Wilaya amemkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri Bib. Pendo Anangisye Malabeja kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo wa kadashi.
Aidha DC amewataka TAKUKURU kuendelea kuchunguza miradi yote ili kama kuna ubadhirifu wa namna yoyote ile uchukuliwe hatua, vilevile amesisitiza kuwa ujenzi wa Kituo cha Afya Kadashi uendelee kwa kasi ili Kituo hicho kikamilike wananchi wapate huduma inayotakiwa.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.