Mpango wa kunusuru kaya masikini ( Tasaf) Leo Machi 22,2023 wamekabidhi mbuzi na kondoo 174 kwa walengwa wa kaya masikini katika Kijiji cha Mwamhembo Kata ya Malya ikiwa ni juhudi za Serikali za kuendelea kuboresha maisha na kukuza uchumi wa Wananchi.
Akikabidhi mbuzi hao Mheshimiwa Athanas Nigo Diwani w Kata ya Malya amewashauri walengwa wote waliopokea mifugo hiyo kwenda kuitunza vizuri Ili iweze kuongezeka na kuwaongezea kipato " hamjapewa hii mifugo Ili mkauze, nendeni mfuge hii ni mbegu kazalisheni Ili mpate mifugo mingi zaidi itawasaidia kuinua uchumi wenu" Nigo
Naye mratibu wa Tasaf Happy Kaali amesema Halmashauri ilipokea fedha kiasi cha millioni 41 kwaajili ya mradi wa kukuza uchumi katika Kijiji cha Mwamhembo na Nyamilama ambapo leo mifugo 174 imetolewa Mwamhembo na mifugo 190 itapelekwa Kwa walengwa wa Kijiji cha Nyamilama
" Leo tumetoa mbuzi na kondoo 174 Kwa vikundi vitano vya walengwa wa Tasaf ambapo Kila Mlengwa amepewa mbuzi au kondoo tatu na tunataraja baada ya muda tutakuta mifugo hiyo imeongezeka kwasababu lengo nikuwawezesha kuongeza kipato na kukuza uchumi, hatutarajii kusikia Mlengwa ameuza hii mifugo kabla haijaongezeka atakayefanya hivyo atakuwa amekiuka utaratibu na ukiukaji wa taratibu unaweza sababisha kufutwa kwenye mpango" Kaali
Kutokana na tukio hilo walengwa wameishukuru Serikali Kwa kuona umuhimu wa kuwapatia mifugo itakayowasaidia kukuza na kuongeza uchumi wao " naishukuru Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kutuletea mifugo hii tunaamini kipato chetu kitaongezeka kutokana na ufugaji huu" amesema Elizabeth Kashinj
Aidha Tasaf inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa, nyumba za watumishi, Zahanati na miradi mingine.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.