Wakala wa huduma za misitu ( TFS) wakabidhi mbao 300 kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ili kuchangangia uboreshaji wa miundombinu ya Elimu.
Akipokea mbao hizo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amesema mbao hizo zitasaidia kutengeneza madawati 200
" kupitia mbao hizi tutatengeneza madawati 200 yale yanayounganishwa kwa vyuma hili litatusaidia kupunguza uhitaji wa madawati katika shule zetu" amesema Msanga
Uongozi wa Halmashauri unaishukuru TFS kwa kuona umuhimu wa kuchangia mbao ili kusaidia uboreshaji wa Elimu, aidha uongozi umeiomba TFS kuendelea kutoa mbao pale zinapopatikana ili kuendelea kuboresha miundombinu ya Elimu.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.