Uongozi wa chama cha Wasiona Wilayani Kwimba umeshiriki zoezi la upandji miti katika Zahanati ya Malemve kata ya Igogwa tarahe 28 Novemba, 2017.Lengo likiwa ni kuwahimiza wananchi kupanda miti katika kaya zao na ili kukabiliana na maafa yanayotokana na ukame.
Akizungumza katika zoezi hilo Afisa maliasili wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Ndg Julius Swai kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji aliwaagiza wananchi wa kata ya Malemve kuhakikisha wanapanda miti ya aina mbalimbali katika Taasisi za serikali na maeneo wanayoishi katika msimu huu wa mvua ili kutimiza mpango wa Halmashauri wa kupanda miti 1,500,000 katika kata 30 za Wilaya ya Kwimba.
Pia Ndg Swai aliiomba serikari kupunguza bei ya Gesi ili wananchi waache tabia ya kukata miti ovyo.
Afisa maliasili wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Ndg Julius Swai akishiriki zoezi la upandaji miti katika Zahanati ya Malemve.
Kwa upande wake Mratibu wa TLB-Kwimba Ndg Isack Manumbu alisema zoezi la upandaji miti ni zoezi endelevu na linamanufaa makubwa katka maisha.
“ kupanda miti ni zoezi endelevu lisihishie hapa kwani linamanufaa makubwa kwa vizazi vyetu na vizazi vya baadaye”
Mratibu wa TLB-Kwimba Ndg Isack Manumbu akishiriki zoezi la upandaji miti
Naye Mwenyekiti wa chama cha watu wasioona Kwimba Ndg Salu Kaswahili amewaomba wananchi kupanda miti na kuitunza.
“Yatupasa kupanda miti na kuitunza kama Mungu alivyopanda bustani na kuitunza upande wa mashariki mwa Edeni”
Aidha Mwenyekiti wa kikundi cha Kazi na Maendeleo kata ya Malemve Bibi Mariam John alisema zoezi za upandaji miti limeleta hamasa kwa wananchi na aliiomba Halmashauri ianzishe kampeni ya upandaji miti katika shule zote za Msingi na Sekondari
Akihitimisha zoezi hilo Mtendaji wa kata ya Igongwa Ndg Robert Emmanuel aliwaomba wadau wengine kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira na elimu ya vitendo kuhusu namna bora ya kupanda miti.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.