" tuendelee kujitoa tuijenge Kwimba yetu" Kauli hii imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga katika kikao cha Kamati ya maendeleo ya Kata ya Nyambiti
Katika kikao hicho Msanga amewashauri viongozi wa Kata hiyo kuendelea kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kujenga maboma ya madarasa, vyoo na miundombinu mingine ambayo yakishafikia hatua ya boma Serikali inaleta fedha kukamilisha.
Aidha Msanga amesisitiza usimamizi wa miradi inayotekelezwa katika Kata hiyo huku akiwataka viongozi kutokuwa vikwazo katika kukamilisha miradi " hatutarajii kuona kingozi ndiye chanzo cha mradi kutokamilika "
Aidha amewataka viongozi hao kutokwepa majukumu yao ya kisheria " hakuna cheo kinaitwa kaimu Mwenyekiti lakini kuna baadhi ya Wenyeviti wametafuta vijana wa kufanya kazi zao, hilo halitakiwi" amesema Msanga
Naye Diwani wa Kata hiyo Mhe. Peter Misalaba amempongeza Mkurugenzi kwa kazi na maelekezo aliyoyatoa pia amemshukuru kwa kupeleka fedha za mapato ya ndani milioni 50 kukamilisha Zahanati ya Mwankuba.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.