Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe. Senyi Ngaga amewataka Wananchi wote kushirikiana na Serikali pamoja na mashirika yanayojishughulisha na Afya kuzuia maambukizi Mapya ya virus vya UKIMWI.
Ameyasema hayo leo Desemba 1,2023 kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani ambapo Mheshimiwa Ngaga alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, maadhimisho hayo yamefanyika Wilayani Sengerema.
" tuendelee kushirikiana kuhakikisha tunazuia maambukizi mapya ya virus vya UKIMWI ili kufikia mwaka 2030 tusiwe na maambukizi kabisa" Ngaga
Mheshimiwa Ngaga amesisitiza kuwa kila mwananchi anapaswa kujikinga na ugonjwa huo na kuwalinda wengine " siku ya leo ni muhimu sana niwaase mjitokeze kupima na unapokutwa na maambukizi siyo mwisho wa maisha"
Aidha Mkuu huyo ameyashauri mashirika mbalimbali kuendelea kutoa Elimu ya kujikinga na VVU huku akiwasisitiza Wananchi kuacha kuwabagua watu wenye maambukizi ya virus vya UKIMWI.
Awali muwakilishi kutoka Wizara ya Afya akiwasilisha taarifa ameishauri jamii kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutokomeza maambukizi mapya ya UKIMWI ukizingatia kauli mbiu ya mwaka huu inayosema " Jamii Iongoze kutokomeza UKIMWI"
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.