"twendeni tukahamasishe jamii kushiriki shughuli za maendeleo"
Kauli hii imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga kwenye vikao vya kamati ya maendeleo ya Kata ya Bungulwa,Walla,Mwagi,Nkalalo na Iseni baada ya kuonekana shule za kata hizo zinaupungufu wa miundombinu.
" maendeleo yanaletwa na mimi na wewe ndio maana ikaitwa Serikali za mitaa, kwahiyo tuhamasishe pia viongozi muwe waaminifu mnapokusanya michango hakikisheni inafanya kazi zilizokusudiwa ili msiwakatishe tamaa wananchi"
Mkurugenzi ametumia mikutano hiyo kuwahamasisha viongozi hao kwenda kutoa elimu ya umuhimu wa kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura.
Vilevile amewataka kusimamia kwa weledi miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yao.
Viongozi wa kata hizo wameshukuru kwa maelekezo yaliyotolewa pia Afisa elimu wa Kata ya Walla Mwalimu Mabosha Malegele amewashauri Walimu Wakuu kuongeza usimamizi wa elimu ili kuongeza ufaulu.
Katika vikao hivyo Mkurugenzi amesisitiza utunzaji wa vyakula ili kuepusha madhara yanayoweza kusababishwa na njaa
Naye Afisa Kilimo wa Kata ya Wala Emida Agostino ameshauri elimu iendelee kutolewa ya umuhimu wa kutunza vyakula " tusaidiane kuelimisha wananchi kutunza vyakula maana familia nyingi zinaathirika pale Baba wa familia wanapochukua vyakula nyumbani wanapeleka kuuza ili kufanya starehe hali inayopelekea familia zao kukosa chakula"
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.