Halmashauri ya wilaya ya Kwimba inayo miradi mbalimbali inayotekelezwa katika vijiji na kata,miongoni mwa miradi hiyo ni ujenzi wa Hospitali ya Wilaya inayojengwa katika kata ya Ngudu eneo la Icheja,ujenzi wa hospitali hii ulianza mwaka 2019 majengo yanatarajiwa kukamilika mwaka 2020.Majengo yanayojengwa katika awamu hii ni jengo la OPD ambalo liko hatua ya renta
jengo la maabara ambalo liko hatua ya msingi
jengo la utawala ambalo liko hatua ya msingi
na jengo la mionzi ambalo liko hatua ya uchimbaji wa msingi
Mpaka sasa pesa iliyopokelewa ni milion 898 kw ajili ya ujenzi wa majengo yote, ujenzi unatarajiwa kukamilika mwaka huu, kukamilika kwa majengo haya kutarahisisha huduma za Afya na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya.Mradi huu ukikamilika utakua miongoni mwa miradi mikubwa inayoendelea wilayani hapa.Miradi mingine inayoendelea ni ujenzi wa zahanati na vituo vya Afya,ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo kwa baadhi ya shule,ujenzi wa visima na matenki ya maji kwa baadhi ya kata,ujenzi wa barabara za mitaa ya ngudu mjini zenye urefu wa km 1.2 kwa kiwango cha rami.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.