Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi amewataka viongozi wa Wilaya hiyo kutilia mkazo ukusanyaji wa mapato ili kuongeza kiwango cha mapato yanayopatikana Wilayani hapo. Mhe. Samizi ameyasema hayo kwenye Baraza la Waheshimiwa Madiwani lililofanyika tarehe 13 May, 2022 katika ukumbi wa Halmashauti ya Wilaya ya Kwimba.
"napenda kuwakumbusha viongozi wote kuwa swala la ukusanyaji wa mapato katika wilaya hii ni jukumu la kila kiongozi na nieleze tu kuwa fedha hizi tusitumie kwa kujinufainisha wenyewe kwani hatua Kali za Sheria zitachukuliwa kwa yoyote Yule kiongozi atakae tumia fedha hizi kwa kujinufaisha "Mkuu huyo akaongezea kwa kuhamasisha swala la ushirikiano katika utendaji kazi" lakini pia niombe sisi Kama viongozi tupende kushirikiana katika Mambo yote yaliyopo ndani ya wilaya" alisema Samizi
Hata hivyo katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Bi.Latifa Malimi amewataka Watumishi Idara ya Afya kufanya kazi kwa upendo na kutimiza wajibu wao kwa weledi
"napenda kugusia upande wa Afya tusimamie vituo vya Afya wagonjwa wapate huduma kwa usahihi na upendo zaidi.pia niwapongeze Sana kamati ya Elimu kwa kupiga hatua kutoka nafasi ya chini mpaka kufikisha ufauru nafasi ya juu kwa Hilo hongereni Sana kamati ya Elimu"
Katika Baraza hilo Bi Happiness Msanga Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba amewasilisha taarifa iliyoonyesha utekelezaji wa miradi mbalimbali na hatua iliyofikiwa, ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa Miradi yote inayotekelezwa ndani ya Halmashauri.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.