Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba Ndugu Nyakia Ally amefanya uzinduzi wa Kituo cha Taasisi ya Elimu ya watu wazima. Kituo hicho kimezinduliwa tarehe 22/12/2021 Katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Ngudu.
Akizindua Kituo hicho Ndugu Nyakia amesema lengo la taasisi kuanzisha kituo cha kutolea elimu ya Stashahada ya Elimu kwa Walimu wa Shule za Msingi ni kuwarahisishia upatikanaji wa Elimu hiyo katika maeneo hayo kwani Hawatahitaji kuomba ruhusa na kwenda kukaa chuoni ili kusoma bali watasoma kipindi cha rikizo tu.
Amewasisitiza Walimu waliojiunga na mpango huo kuitumia fulsa hiyo kusoma kwa bidii ili kujiongezea ujuzi kutokana na Elimu hiyo, pia kujiendeleza ili hatimae waweze kupata alama zitakazowawezesha kusoma Shahada.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amewataka Walimu hao kuso kwa bidii, kuitumia fulsa hiyo kujipatia Elimu kwa gharama nafuu na amewasisitiza kupangilia mda wao vizuri ili masomo yao yafanikiwe na kazi ziendelee kwa ufanisi.
" mnachukua Diploma ya Elimu msilizike, tumieni hiyo diploma mtakayoipata kama daraja la kupata degree" amesema Msanga
Katika hafla hiyo Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu wazuma Mwalimu Taison amesema Taasisi imeamua kuanzisha kituo katika wilaya ya Kwimba baada ya kugundua kuna Walimu wengi wanaohitaji kujiendeleza lakini wengi wao wanapata changamoto ya kwenda kukaa Vyuoni kusoma, hivyo kuanzisha kituo hapa kwimba kutawawezesha kusoma huku wakiendelea na kazi zao za kila siku.
Aidha Afisa Elimu Msingi Mwalimu Mabeyo Bujimu ameushukuru uongozi wa Wilaya kwa kukubali uanzishwaji wa kituo cha kutolea Stashahada ya Elimu ya watu wazima kwani kituo hicho kinalenga kuwainua Walimu wengi ambao walikuwa bado hawajajiendeleza.Pia amewasisitiza Walimu kuitumia nafasi hiyo vizuri ili kutimiza malengo yao ya kupata stashahada ya Ualimu na kisha wasikomee hapo wajiendeleze zaidi.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.