Mhe.Senyi S. Ngaga Mkuu wa Wilaya ya Kwimba amepandikiza vifaranga elfu ishirini vya samaki aina ya sato katika bwawa la maiga Wilayani Kwimba,vifaranga hivyo vimetolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.Zoezi hilo limefanyika leo tarehe 26/10/2020.
Akiongea na wananchi waliohudhuria tukio hilo amewataka kulinda bwawa hilo ili samaki hao waweze kukua na wavuliwe kwa wakati sahihi.
Juhudi hizi za kutaka kuongeza upatikanaji wa samaki Wilayani hapa zinatokana na uhitaji wa samaki kuwa mkubwa kuliko upatikanaji wake,Wilaya ya Kwimba iko Mkoa wa Mwanza, Mkoa ambao unaziwa kubwa lakini Wilaya hii Haina ziwa wala mto mkubwa hivyo viongozi wa Wilaya hii wameona watumie fursa ya bwawa hilo la maiga kufugia samaki ili kuongeza kitoweo hicho Wilayani hapa pamoja na kuongeza mapato ya Halmashauri.
Wataalamu wa mifugo waliohudhuria tukio hilo wamesema samaki hao watakuwa tayari kuvunwa baada ya miezi 6 na kuendelea
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.