Ikiwa ni utaratibu wa baraza la Madiwani kuchagua makamu Mwenyekiti kila mwaka na wajumbe wa kamati mbalimbali ikiwemo kamati ya Elimu na Uchumi, leo tarehe 7, Sept 2022 Madiwani wamemchagua Hole Mashauri Diwani wa Kata ya Mantare kuwa Makam Mwenyekiti na madiwani wengine wamechaguliwa kuongoza kamati mbalimbali ikiwa ni pamoja na kamati ya uchumi na Elimu.
Kabla ya uchaguzi huo Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi amewataka madiwani hao kuchagua viongozi watakaoweza kuisaidia Halmashauri kufikia malengo ya maendeleo
“tunatarajia kuona viongozi watakaochaguliwa wawe niwale ambao wakotayari kufanyakazi kwa maslahi ya Serikali,watu watakaoisaidia Halmashauri kufikia malengo, viongozi watakaofanya kazi za maendeleo siyo kuleta migogoro” amesema Samizi
Baada ya maelekezo hayo Mheshimiwa Hole Mashauri alipewa nafasi ya kujinadi kwa madiwani ili waweze kumchagua kuwa Makam Mwenyekiti ambapo nafasi hiyo ameitumia vyema kuwataka madiwani wote bila kuzingatia vyama vyao kumchagua jambo ambalo limefanikiwa kwa kiwango kikubwa kwani baada ya kura kupigwa,kura zote zilikuwa za ndiyo ikimaanisha madiwani wote wamekubaliana naye.
Aidha baada ya uchaguzi huo Mkuu wa Wilaya amewapongeza viongozi wote waliochaguliwa na amewataka kufanya kazi kwa upendo na ushirikiano ili kuchochea ari ya maendeleo na kutatua changamoto za wananchi.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.