Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga amefanya kikao na Serikali ya Kata ya Malya,Lyoma na Mwandu ambapo amewataka viongozi wa vijiji na Kata kuhakikisha wanazingatia Sheria na taratibu zinazoongoza Serikali ngazi ya Kijiji na Kata.
Bi. Msanga amewataka kufanya vikao na mikutano ya kisheria ili wananchi wapate nafasi za kutoa kero zao na changamoto.Pia amewasisitiza kusoma mapato na matumizi ili wananchi wawe na taarifa sahihi za mapato ya maeneo yao.
Aidha amewataka Wenyeviti wa Vijiji na vitongoji kuhamasisha wananchi kujitokeza kuboresha Taarifa zao kwenye daftari la kudumu la wapiga kura pindi kazi hiyo itakapoanza ili kuepusha changamoto za kukosa jina au jina kukosewa kwenye daftari wakati wa uchaguzi.
Bi. Msanga amewataka viongozi wa Kata hizo kuhakikisha wanashirikiana kusimamia miradi inayotekelezwa katika maeneo yao.pia amewasisitiza kuhamasisha wananchi kuongeza miundombinu ya Shule hasa kuanzisha maboma ya madarasa na vyoo.
Viongozi hao wamehamasishwa kuhusu utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti na kuitunza" tutunze mazingira ili yatutunze" pia wamehamasishwa kuwalinda watoto wa kike na kuhakikisha wanawasomesha.
Katika vikao hivyo ameshiriki Mkuu wa kitengo cha huduma za Sheria Denis Kabogo ambaye amewaelekeza Sheria mbalimbali zinazoongoza utendaji kazi ngazi ya Kijiji na Kata.
Naye Afisa rasilimali watu Ndugu Reginald Clavery amewakumbusha majukumu yao kuanzia Mwenyekiti wa kitongoji hadi Mtendaji wa Kata ili kuwasaidia kutoingilia majukumu ya mtu mwingime.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.