Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe.Johari M.Samizi amewataka viongozi wa ngazi zote ndani ya Wilaya kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo kwa umakini na weredi wa hali ya juu.Haya ameyasema katika Mkutano wa Baraza la Madiwani robo ya nne mwaka 2020/2021 uliofanyika tarehe 18 Agosti,2021 kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.Mkuu huyo ameyasema hayo kutokana na ziara aliyoifanya wiki iliyopita ya kutembelea miradi inayotekelezwa na kukuta badhi ya miradi kutokuwa na ubora unaotakiwa.Amewasisitiza Madiwani kufanya kazi kwani muda wa Kampeni ulishapita sasa ni kazi tu "muda wa kampeni umekwisha twendeni tukafanye kazi,tusijaribiane kwenye kazi,hili ndilo shamba langu sitarajii mtu kunivurugia Shamba,hatutarajii mtu yeyote kuvuruga kazi inayoendelea" amesema Johari
Aidha Mhe. Johari amejitambulisha kwa Waheshimiwa Madiwani kwani baadhi yao alikuwa bado hajakutana nao, kisha amewaomba ushirikiano kwa kipindi chote atakacho tumika kama Mkuu wa Wilaya ya Kwimba. Amewasisitiza Madiwani kutoa Elimu ya ugonjwa wa COVID 19 kwa Wananchi na kuwahamasisha wananchi kwenda kuchanjwa ili kuboresha kinga dhidi ya virus vya corona.
Bi.Happiness J.Msanga Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba
Katika Mkutano huo wenyeviti wa kamati mbalimbali wametoa taarifa za shughuli zinazoendelea katika kamati zao ambapo hoja mbalimbali zimeibuka ikiwemo Shule zisizo na Walimu wa Kike zitafutiwe ufumbuzi,uvuvi haramu katika bwawa la Mahiga udhibitiwe na kamati ya fedha ifanye ziara kwenda kujifunza utaratibu unaofanyika katika Mikoa inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ili wapate ujuzi wa kusimamia uchimbaji wa madini unaofanyika katika Wilaya ya Kwimba kwani shughuli hiyo imeonekana kusuasua katika ukusanyaji wa mapato.
Mkutano huo umehudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Kwimba ambaye amewakaribisha Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi katika Wilaya ya Kwimba kwani viongozi hao ni wageni, kisha ameshauri usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya ya Kwimba.
Mansoor S.Hiran(MB) Jimbo la Kwimba
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.