Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike amewataka viongozi kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa madarasa 109,Vituo vya Afya, madaraja na ujenzi wa matanki ya maji huku wakizingatia utunzaji wa mazingira.
Ameyasema hayo leo tarehe 12/11/2021 wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa wilayani Kwimba. Akikagua ujenzi wa madarasa katika Shule za Sekondari Bungulwa, Walla na Ngula ameshauri ujenzi wa madarasa hayo uzingatie ubora na thamani ya fedha ionekene baada ya majengo hayo kukamilika kwa wakati, katika usimamizi wa miradi hiyo amesisitiza uaminifu na uadirifu.
Pia amewataka kuhakikisha wanapanda miti ya matunda na ya vivuli katika mazingira ya Shule ili kutengeneza uhalisia wa kile walimu wanachokifundisha lakini kupanda miti katika maeneo mengine ili kutunza mazingira na kupambana na mabadiriko ya hali ya hewa, amesisitiza kuwa hali ya Kwimba inatakiwa kubadirika kwa kupanda miti mingi katika maeneo yote.
Katika ziara hiyo Samike amekagua ujenzi wa daraja kata ya Walla na kumtaka mhandisi kuendelea kusimamia ubora wa daraja hilo vilevile amewataka wahandisi kuongeza kasi ili daraja likamilike na kuanza kutumika.
Aidha Katibu Tawala huyo amefika kwenye mradi wa tanki la maji unaotekelezwa na wakala wa maji vijijini RUWASA na kuwataka kufika Disemba mradi huo uwe umekamilika ili wananchi waanze kupata huduma ya maji katika kijiji hicho.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.