Kampuni ya Mtandao wa simu Vodacom limekabidhi matundu 14 ya vyoo katika Shule ya msingi Mwalujo iliyopo Kata ya Mwamala Wilayani Kwimba.
Akikabidhi Mradi huo Ndugu Agapinus Tax Mkurugenzi wa vihatarishi na ithibati wa Vodacom amesema Vodacom inaedelea kutekeleza miradi katika maeneo mbalimbali ya Tanzania ambapo kwa Wilaya ya Kwimba Vodacom imejenga matundu 14 ya vyoo yenye thamani ya milioni 160
"msaada huu ni pamoja na juhudi za Vodacom kuunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha utoaji wa Elimu Kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuwaboreshea mazingira ya kujifunza maana kila mtoto ana haki ya kupata Elimu bora kwahiyo inatakiwa iwe Elimu bora kwenye mazingira safi na salama" mesema Taxi
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Bi. Rozalia Magoti akipokea mradi huo ameishukuru kampuni ya Vodacom kwa ujenzi huo wa vyoo na amewaomba wasiishie hapo waendelee kuleta misaada ya namna hiyo Ili kuendelea kuboresha Elimu. Pia amewataka wanafunzi na Walimu kuhakikisha wanatunza miundombinu hiyo Ili iweze kutumika kwa kipindi kirefu kama ilivyokusudiwa
Wanafunzi wa Shule hiyo pamoja na Walimu wao wamefurahi sana na wameishukuru Vodacom kwa kuona umuhimu wa kujenga vyoo katika Shule yao
" tunaishukuru Vodacom kwa kutujengea vyoo maana tulikuwa na vyoo vibovu sana lakini sasa tumepata vyoo vya kisasa tunaahidi kuvitunza" amesema Mwanafunzi Jacob Simon Mteka
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.