Wadau mbalimbali wa Chama cha Watu Wasioona Kwimba wamefanya kikao cha kimkakati tarehe 3-4/ Januari, 2018 katika ukumbi wa Klasta Kakola. lengo likiwa ni kuendea kutekeleza Mradi wa Ushawishi, Uzengezji na Utetetezi kwa watu wenye ulemavu ili kushiriki katika fulsa mbalimbali katika maamuzi na kupatiwa haki zao.
“Tanzania ni nchi iliyojengwa kwa kufuata misingi ya usawa na haki kwa wananchi wote. kila mwananchi ana haki sawa kisheria ya kushiriki kikamilifu katika mambo muhimu yanayomuhusu yeye mwenyewe na jamii nzima kwa ujumla hivyo watu wenye ulemavu wana haki ya kupata mahitaji ya msingi kama watu wasiyo na ulemavu hivyo basi tusiwatenge”.
Hayo yalisemawa na Mratibu Chama cha Wasioona Kwimba Ndg Isack Manumbu wakati akiutambulisha Mradi kwa wadau wa Chama Cha Wasioona.
Akiongea katika kikao hicho Mkuu wa kitengo cha Elimu Malaalum Bibi Elizabeth Tenga aliishauri jamii kuachana na mira potofu kwa watu wenye Ulemavu ambapo baadhi ya wazazi na walezi kuwaona watoto wenye ulemavu kama mzigo hivyo kutowapeleka Shule.
Mkuu wa kitengo cha Elimu Malaalum Bibi Elizabeth Tenga akichangia mada wakati wa kikao
Kwa upande wake Ndg Shija Spea Mdau kutoka Kibitilwa aliiomba Serikali kuhakikisha inawapatia watu wenye ulemavu nyezo za kujimudu ambazo zinaweza kuwawezesha kufika katika vituo vya afya kwa urahisi ili kupata huduma za afya wanazostahili.
Akienelea kuchangia Mwl Asia Khamisi kutoka shule ya Msingi Kakola aliiomba Serikali na Jamii kwa ujumla kuhakikisha inaboresha miundombinu katika sehemu za kutolea huduma ili kupunguza changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu.
Kwa kuongezea Ndg Jonson Muyombya mwezeshaji wa kikao mkakati kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba alisema wadau wote wa Chama cha Wasioona Kwimba tuhakikishe tunatumia nafasi zetu vizuri.
“Tuhakikishe tunatumia nafasi zutu vizuri katika kutekeleza haki za watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kuwapenda,kuwaheshimu,kuwatunza na kuwathamini”.
Ndg Muyombya aliendelea kuchangia kwa kuwakumbusha wadau wote kuwa tuhakikishe tunaenda kuwa marafiki wa walemavu na siyo kuwa maadui kwenye jamii tunazoishi.
Baadhi wa Wadau wa Chama cha Watu Wasioona Kwimba wakijadili Mada katika Makundi.
Naye Mwl Mariam Maguli kutoka kitengo cha Elimu Maalum katika shule ya Msingi Kakola aliishauri jamii kuwapeleka watu wenye ulemavu katika vyuo vya ufundi vinavyotoa mafunzo ya stadi za kazi kwani yanampa mtu mwenye ulemavu nafasi ya kupata ajira.
Wadau mbalimbali wa Chama cha Wasiona chini Mradi wa " Ushawishi, Uzengezji na Utetetezi kwa watu wenye ulemavu ili kushiriki katika fulsa mbalimbali katika maamuzi na kupatiwa haki zao" Wilayani Kwimba wametoka katika kata ya Igongwa, Mwagi, Bungulwa, Nkalalo, Iseni, Nyambiti, Ngh’undi, ,Mwakilyambiti na Ilula Wilayani Kwimba.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.