Wadau wa kuzuia na kupambana na Rushwa wamedhamiria kutokomeza Rushwa kwa kutoa elimu ya madhara ya rushwa kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa, majukwaa mbalimbali yanatarajiwa kutumika kuelimisha wananchi.
Haya yamejiri kwenye Semina ya wadau wa kuzuia na kupambana na Rushwa iliyofanyika leo Septemba 4,2024 kwenye ukumbi wa Klasta.
Akiwasilisha mada ya semina hiyo Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Kwimba Julian Augustine amesema madhara ya rushwa kwenye kipindi cha uchaguzi yanaweza kupelekea jamii kupata viongozi ambao siyo chaguo la Wananchi wengi.
" jukumu la kupambana na rushwa ni la wananchi wote kwahiyo niwaombe viongozi wa dini tumieni madhehebu yenu kuelimisha wananchi madhara ya rushwa" Juliani
Kamanda Juliani ametumia wasaa huo kuvitaka vyombo vya Habari kutumia teknolojia ya habari kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya rushwa.
Nao wadau wamepanga mikakati ya kwenda kutoa elimu kwa wananchi na kutoa taarifa kwa vyombo husika pindi watakapoona viashiria vya rushwa mahali popote.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba akijitambulisha kwa kundi hilo la viongozi wa dini, wawakilishi wa vyama vya siasa, vyombo vya Habari na Asasi za Kiraia ameomba ushirikiano katika kutekeleza shughuli mbalimbali za serikali.
Semina hiyo iliyokuwa na kauli mbiu inayosema " kuzuia rushwa ni jukumu langu na lako,tutimize wajibu wetu" imewaandaa wadau hao kwenda kuwa waelimishaji.
Katika semina hiyo ameshiriki Afisa uchaguzi wa Halmashauri Ndug Reginald Clavery ambaye ameeleza kanuni zinazoongoza uchaguzi wa Serikali za mitaa, sifa za mpiga kura na sifa za mgombea.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.