Mwenyekiti wa Baraza la biashara ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Mussa Samizi amewashauri wafanya biashara wa Wilaya hii kuanzisha viwanda vya kusindika na kutengeneza vitu mbalimbali vitakavyochochea maendeleo katika Wilaya ya Kwimba. Haya yamejitokeza kwenye mkutano wa baraza la biashara uliofanyika tarehe 31,Agosti 2021 kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.
Katika baraza hilo Daktari Farid Saleh amewashauri wafanyabiashara kuanzisha kiwanda cha kutengeneza dripu kwaajili ya matumizi ya Hospitali, zahanati na Vituo vya Afya ameshauri kuwa endapo vifaa vitapatika Wilayani itapunguza gharama za kuvisafirisha kutoka mbali, pia itachagiza maendeleo kwani vijana wengi watapata ajira katika viwanda hibyo.Amesisitiza kuwa mfanyabiashara atakayeanzisha kiwanda hicho atapewa ushirikiano wa kitaalamu na Wataalam wa Afya.
Aidha Meneja wa TRA Ndug. Mihayo K.Mitili ametoa elimu kuhusu kodi ya majengo inayokatwa kupitia LUKU Tanesco. Amesema wamiliki wa nyumba zenye mita zaidi ya moja wafike ofisi za TRA hapo watapewa fomu za kujaza zitakazoonyesha mita ipi itumike kulipia kodi ya jengo kati ya hizo mita zote endapo wamiliki hawatajaza fomu hizo mita zote zitakatwa kodi ya jengo. Meneja ameshauri wananchi kufika ofisini kwake ili kupa maelekezo zaidi kuhusu kodi za majengo.
Baraza hilo limehudhuliwa na kiongozi wa stesheni (Station Master) wa Bukwimba Nkalalo Ndug. Omari Simwanga, yeye amewashauri wafanyabiashara kujenga majengo ya biashara na nyumba za wageni pale Nkalalo kwani reli ya kisasa (SGR) itakapokamilika eneo hilo litakuwa na watu wengi ambao watahitaji huduma za hoteli,nyumba za kupanga, huduma za kifedha( benki), usafiri na mahitaji mengine mengi hivyo amewasihi wafanyabiashara kuiona hiyo kama fursa kwao ya kwenda kuwekeza Nkalalo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.