Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi amewashauri wafanyabiashara na wajasiliamari kugeuza changamoto kuwa fulsa. Ameyasema hayo kwenye balaza la Wafanyabiashara lililofanyika tarehe 8,Aprili 2022 kwenye ukumbi wa Chama cha Walimu.
Mkuu huyo amesema Wilaya ya Kwimba inayo maeneo makubwa ambayo yanatosha kuanzisha viwanda vya kuchakata mazao na bidhaa mbalimbali, hivyo amewashauri wafanyabiashara kuchukua changamoto za ukosefu wa bidhaa mbalimbali kama fulsa ya kuanzisha viwanda vitakavyopelekea upatikanaji wa bidhaa hizo.
Pia amesisitiza kuwa Wananchi wapewe Elimu juu ya umuhimu wa kilimo cha zao la Alizeti ili zao hilo lilimwe kwa wingi ili wafanyabiashara wanapoamua kuanzisha mashine za kukamua mafuta ya Alizeti maligafi iwepo.
"tuhamasishane kwamba pamoja na kulima mazao mengine kama Pamba, choroko, dengu na Mpunga tulime na alizeti kwa wingi tena iwekwe sheria ya kila kaya kulima heka mbili za Alizeti"
Katika balaza hilo wadau wa biashara wakiwemo wawakilishi wa Taasisi za Kibenk wamewashauri wafanyabiashara na wakulima kufika benki ili kupata mikopo yenye lengo la kumuinua Mkulima na mfanyabiashara wa bidhaa zitokanazo na kilimo.
Aidha Mkuu wa Wilaya ameshauri wafanyabiashara ndogondogo kuwekewa miundombinu wezeshi kama umeme, mpangilio mzuri wa vibanda ili kuwarahisishia biashara zao.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.