Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija amewashauri wafanyabiashara kushirikiana na Serikali ili kurahisisha huduma wanazotoa na kujenga uchumi
" wajumbe mlioshiriki baraza hili nendeni mkawe mabalozi kwa wafanyabiashara wengine, kinachotakiwa ni kushirikiana sekta binafsi na sekta za umma ili kuongeza tija katika biashara na kujenga uchumi wa Wilaya na Taifa kwa ujumla" Ludigija
Mheshimiwa Ludigija aliyasema hayo katika kikao cha Baraza la Biashara Wilaya ya Kwimba lililofanyika tarehe 20 Novemba, 2023 katika ukumbi wa Halmashauri ambapo wajumbe mbalimbali walishiriki wakiwemo wafanyabiashara na viongozi wa Taasisi mbalimbali.
Katika baraza hilo watumishi wa Idara ya Afya wameshauriwa kuwa wabunifu kwa kuanzisha viwanda vidogovidogo vinavyoweza kuzalisha bidhaa mbalimbali kama vile drip za maji, pamba na vitu vingine.
Aidha wajumbe wa Baraza hilo wamemshauri Mwenyekiti wa wafanyabiashara Wilaya kuwaunganisha wafanyabiashara na Serikali na kuhakikisha anatatua migogoro ili wafanyabiashara wafanye kazi zao bila usumbufu
" Mimi nishauri Mwenyekiti wetu wa Wilaya atuunganishe na Serikali hii itakuwa rahisi hata kuondoa migogoro inayojitokeza baina ya wafanyabiashara na Halmashauri sisi tunataka kufanya biashara bila usumbufu " amesema Masumbuko Shigita
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.