Bi. Shamimu Mwanamalunde Mganga wa tiba asili, mkazi wa Wilaya ya Kwimba amefanyiwa upasuaji na kutolewa uvimbe wenye uzito wa kilo 2.5 aliodumu nao kwa zaidi ya miaka 20.
Akiongea Hospitalini hapo Juni 19,2024 mara baada ya kupatiwa matibabu amesema uvimbe ulianza kama mimba ya miezi miwili lakini haikuendelea kukua tangu kipindi hicho
" sikumbuki ni mwaka gani lakini mwanangu wa kike alikuwa darasa la tano na hivi sasa alishamaliza shule na ameolewa na anawatoto wanane" amesema Mwanamalunde
Mwanamalunde ameongeza kuwa pamoja na kwamba yeye ni mganga wa tiba asili lakini hakuweza kujiganga kwa kipindi chote hicho
"niliposikia wamekuja hawa wataalamu wa Samia, nilifurahi nikaja wamenipima na kunifanyia upasuaji na wametoa uvimbe" Mwanamalunde
Kwa upande wake Mganga mfawadhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kwimba Bi. Neema Gervas amesema kambi ya Madaktari bingwa imekuwa na matoleo chanya
"siku za kawaida huwa tunapokea wagonjwa 60 hadi 70 kwa siku lakini ujio wa madaktari bingwa umeongeza idadi hadi 130 kwa siku"
Naye Daktari Bingwa wa upasuaji Lesso Mwinyimkuu amesema toka kuanza kambi hiyo wamefanya upasuaji ambao ungehitaji rufaa ya Hospitali ya Mkoa au kanda"
Madaktari Bingwa watakuwepo Kwimba wakitoa huduma hadi tarehe 21 Juni, 2024
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.