Viongozi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Malya wamefanya mahafali ya 44 ambapo katika mahafali hiyo jumla ya wanachuo 237 wamehitimu. Katika mahafali hiyo iliyofanyika tarehe 11/11/2021 wahitimu wameweza kuonyesha ujuzi wa fani mbalimbali wanazofundishwa chuoni hapo.
Wahitimu wa ufundi wa magari wameweza kuonyesha jinsi ya kutengeneza magari mabovu, waliojifunza umeme wameonyesha jinsi wanavyoweza kufunga umeme wa viwandani na majumbani na wahitimu wa fani nyingine wameonyesha ujuzi walioupata.
Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Malya kinatoa kozi mbalimbali ikiwemo umeme, ufundi magari, fundi bomba, fundi wa kushona nguo, mifugo, fundi washi na waalimu wa malezi ya watoto wadogo.
Aidha chuo hicho kinatoa elimu ya Sekondari (elimu haina mwisho yaani QT) kwa wasichana walioshindwa kupata elimu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mimba za utotoni, kusitisha masomo kwa sababu ya ugonjwa au sababu nyingine. Wasichana hao wanapata elimu ya sekondari bure na wanafundishwa na fani nyingine. Elimu hiyo ya sekondari inatolewa kwa miaka miwili tu ambapo kidato cha kwanza na chapili wanasoma kwa mwaka mmoja na kidato cha tatu na nne wanasoma mwaka wa pili.
Mgeni rasmi wa Mahafali hayo alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kwimba Ndug. Nyakia Ally ambaye amemshauri Mkuu wa Chuo Mwalim Frenk J Igembe kuanzisha Shule ya msingi kwamaana ya ( english medium ) kwa sababu walimu anawatengeneza yeye mwenyewe, pia ameshauri na fani nyingine ziongezwe na hizo zilizopo ziendelee kutoa wataalam wa kutosha ili wakafanye kazi za kuleta maendela kwenye Taifa letu.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.