Shirika la SIDO (small Industries Development Organization) limeendesha mafunzo ya siku tano ya usindikaji wa vyakula vya aina mbalimbali kwa Wajasiriamali wa vikundi vilivyopewa na vinavyotarajiwa kupewa mikopo na Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, mafunzo hayo yamefunguliwa na Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Ruth Malisa kwa niaba ya Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya huku akiwasisitiza Wajasiriamali hao kujifunza kwa umakini ili wapate ujuzi utakaowasaidia kujiongezea kipato kutokana na mikopo wanayopewa.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa vitendo, Katika Mafunzo hayo Wajasiriamali wamejifunza kusindika vyakula mbalimbali ikiwemo Mikate, Keki, Unga wa lishe, Biskuti, Tomato, Maziwa mgando, Karanga na mengine.
" Tumejifunza kutengeneza vitu vingi ambapo ujuzi huu tunatarajia kwenda kuutumia katika kujiongezea kipato, tunatamani siku moja kuanzisha kiwanda kikubwa cha kutengeneza mikate hapa Kwimba kwahiyo tutaanza taratibu ila tunamalengo makubwa" amesema Angela Mahiga mnufaika wa mafunzo
Aidha Meneja wa SIDO Mkoa wa Mwanza Ndug.Bakari A. Songwe akifunga mafunzo hayo amewataka Wajasiriamali kwenda kutumia ujuzi walioupata katika kuwaletea maendeleo ya Familia na Jamii kwa ujumla.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.