Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa kijiji cha Mhulya kutoka 40% hadi 90% kutokana na kuwajengea mradi wa maji wenye thamani ya Tshs. 667.1 milioni fedha za mfuko wa maji wa Taifa.
Mhe. Mtanda ametoa pongezi hizo leo tarehe 14, 2024 katika kijiji cha Mhulya kilichopo kwenye kata ya Ngula wakati akikagua mradi wa maji kutoka kwenye chanzo cha kisima kirefu cha mita 80 chenye uwezo wa kuzalisha maji lita 12,336 kwa saa ambao umekamilika tangia mwezi juni 2023 chini ya usimamizi wa RUWASA.
Aidha, amewataka wananchi kulinda miundombinu ya mradi huo na viongozi wanaosimamia jumuia ya watumia maji kuketi na wananchi na kukubaliana nao juu ya bei ya kuuziana maji kwenye mradi huo kama uchangiaji wa huduma na fedha zinazopatikana zitumike kufanya ukarabati na marekebisho ya miundombinu itakapohitajika.
Vilevile, amewahamasisha wananchi hao kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura na kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika i novemba 27, 2024 ikiwa ni pamoja na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba 2025.
Meneja RUWASA wilaya ya Kwimba Mhandisi Godliver Gwambasa amesema mkandarasi KPR ameshakamilisha kazi na maji yanatoka kwenye vituo vyote 9 vya kuketea maji kwenye kijiji hicho na mradi huo kwa sasa unaendeshwa na wananchi wenyewe chini ya chombo cha kuendeshea maji (CBWSO) cha kijijini hapo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.