Mkimbiza Mwenge Kitaifa Ndugu Sahili Nyanzabara Geraruma awapongeza viongozi wa Wilaya ya Kwimba kwa kusimamia,na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ufanisi na ufasaha.Ndugu Geraruma ameyasema hayo wakati akikagua miradi tisa,ambapo miradi mitatu imekaguliwa,miradi mitatu imewekewa mawe ya msingi na miradi mitatu imezinduliwa.
Mwenge wa Uhuru umepokelewa leo tarehe 12,Julai 2022 katika Kijiji cha Mwamhembo kata ya Malya umekimbizwa kilomita 124.8 na umekagua miradi hiyo yenye jumla ya bilioni 3.82. Katika mbio hizo mwenge ulianza kwa kukagua mradi wa programu maalumu ya mafunzo kwa wanafunzi wakike waliokatisha masomo baada ya kupata ujauzito katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Malya. Katika Chuo hicho wakimbiza mwenge wamewapongeza wanafunzi wote wanaosoma katika chuo hicho na wameshauri kusoma kwa bidii ili wafikie malengo yao.
Aidha mwenge huo umekagua mradi wa anwani za makazi katika kijiji cha Malya ambapo jiwe la msingi limewekwa katika mradi huo, Kisha Mwenge umekagua na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa tangi la maji lenye ujazo wa lita 135,000 katika kijiji cha Ibindo.Mwenge huo haukuishia hapo umeweka jiwe la Msingi katika mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya katika kijiji cha Isunga.
Mwenge wa Uhuru umezindua madarasa matano katika Shule ya Sekondari Walla,umezindua daraja la Walla na umezindua madarasa sita katika Shule ya Msingi Kabale ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kupitia mapato ya ndani imeweza kujenga madarasa ya kisasa sita baada ya madarsa yaliyokuwepo katika Shule hiyo kuchakaa na kutofaa kwa matumizi. Katika miradi hiyo wakimbiza mwenge wamepongeza jitihada zilizofanya na Halmashauri ili kufanikisha ujenzi hio katika Shule ya Msingi Kabale.
Katika mbio hizo wakimbiza Mwenge wa Uhuru wamesisitiza kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2022 inayosema”Sensa ni msingi wa mipango ya maendeleo,shiriki kuhesabiwa tuyafikie maendeleo ya Taifa” aidha wakimbiza Mwenge hao wametoa elimu kwa Wananchi juu ya umuhimu wa Sensa ya watu na makazi,wamesisitiza lishe kamili kwa watu wote ili kuepukana na udumavu na utapiamlo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.