Mkuu wa wilaya ya Kwimba Mhe: Senyi S Ngaga awataka AMCOS ( Agricultural Marketing Cooperative Society )kulipa pesa za wakulima kwa wakati pindi tu pesa inapowekwa kwenye akaunti na amewaonya viongozi wa AMCOS wanaokaa na pesa za wakulima kwa mda mrefu kuwa hatua Kali zitachukuliwa. Haya yamejitokeza katika kikao cha Mkuu wa wilaya, AMCOS na Maafisa Ugani kilichofanyika tarehe 14/02/2020 katika ukumbi wa Halmashauri,aidha Mkuu wa wilaya ametaka kujua madeni yote ya wakulima wa pamba kutoka kwa kila AMCOS na madeni ambayo AMCOS wanadai kwa makampuni yanayonunua pamba.
Aidha Mhe: Ngaga amewataka viongozi wa AMCOS kuwahamasisha wakulima kufungua akaunti ili kurahisisha malipo na kuongeza usalama wa pesa za wakulima .
Katika kikao hicho Meneja wa NMB na CRDB wameelezea faida za kufungua akaunti ya mkulima kua ni akaunti ambayo haina makato ya kila mwezi hivyo wakulima wasiogope kufungua akaunti.
Viongozi wa AMCOS wamewaomba mameneja hao kwenda vijijini kutoa elimu kwa wakulima ili kuonyesha umuhimu wa akaunti hizo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.