Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe.Johari Samizi amewataka wakulima kutochanganya mazao mengine na Pamba. Ameyasema hayo jana tarehe 08/11/2021 baada ya kutoa Elimu ya kilimo cha Pamba kwa Wananchi wa Kata za Lyoma, Mwankulwe na Mwakilyambiti
Mheshimiwa Samizi amesisitiza hilo baada ya Balozi wa Pamba Mhe. Aggrey Mwanri kuwafundisha Wakulima kutochanganya zao la Pamba na mazao mengine, kwani kuchanganya pamba na mazao mengine kunapelekea wadudu wanaoshambulia mazao hayo kushambulia na Pamba.
Mheshimiwa Aggrey Amesema kama wakulima watachanganya Pamba na mazao mengine hawataweza kufikia lengo la kupata kilo 2500 kwa Ekari moja kwani kuchanganya mazao kunaifanya pamba inashindwa kukua na kuongeza vitumba vingi zaidi kwa mche mmoja.
Aidha Mhe.Aggrey amewafundisha Wananchi kanuni kumi za kilimo bora cha Pamba ikiwa ni kutayarisha shamba mapema,Tumia mbolea na virutubisho vingine,Panda Pamba mapema,Panda kwa mistari na kwa vipimo vya sentimita 60 kwa 30 ,Panda idadi halisi ya mbegu katika kila shimo( mbegu tatu hadi tano),Punguzia miche,Palilia kwa wakati,Nyunyizia madawa kuzuia wadudu,Vuna pamba mapema na chambua na Ng'oa na choma moto masalia yote ya pamba.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.