Walengwa wa Kaya masikini (TASAF) washauriwa kutumia fedha wanazopata kujiongezea kipato. Ushauri huu umetolewa na wawezeshaji wa Tasaf wakati wa zoezi la kuwapatia fedha za mpango wa kunusuru kaya masikini lililo fanyika kuanzia tarehe 18 Mei 2022 hadi 24 Juni 2022.
Walengwa hao wameshauriwa kutumia fedha kwa malengo yaliyokusudiwa ikiwemo kuwanunulia wanafunzi sare za shule, madaftari na vitu vingine muhimu.
Aidha walengwa wameshauriwa kufanya vitu vinavyoweka kumbukumbu kama kununua bati za kujengea, kujenga nyumba bora, kuanzisha ufugaji na vitu vingine
" nunueni Ng'ombe, mbuzi, kondoo na kuku tumieni hii fedha kufanya vitu vinavyoonekana na vitakavyowaongezea kipato" alisema Awalina Majidu muwezeshaji
Katika mwezi huu wa Machi- April jumla ya shiling 401,646,026 zimetolewa kwa kaya 8821 za walengwa wa Tasaf.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.