Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness J. Msanga amewataka Walimu Wakuu kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza kazi zao.
Ameyasema hayo jana tarehe 7,Disemba 2022 katika kikao cha robo mwaka cha Walimu wakuu kilichofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Ngudu.
“ acheni kufanya kazi kwa mazoea, nendeni mkabadirike sisi ni watumishi wa umma lazima hilo mlitambue kuwa nyie ni kiyoo katika jamii kwahiyo msidharirishe utumishi wenu, waambieni na Walimu mnaowasimamia”
Akisisitiza nidhamu,uwajibikaji na suala la kutunza siri amewataka Walimu kuwa na falagha siyo kuweka wazi kila kitu hata ambayo hayatakiwi kuwekwa wazi.
Vilevile walimu Wakuu wameelekezwa kuanzisha mashamba lishe katika Shule zao ili kuboresha Afya za wanafunzi kwa kuwapatia chakula Shuleni
“nendeni mkaanzishe mashamba ya lishe mkalime mahindi lishe, viazi lishe na mbogamboga ili visaidie kupatikana kwa chakula shuleni lakini mkawaelimishe na wazazi wa wanafunzi juu ya umuhimu wa chakula shuleni” amesema Msanga
Katika kikao hicho Walimu Wakuu wametakiwa kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Shule zao, wamesisitizwa kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa
“simamieni miradi ya maendeleo kwa umakini, sina urafiki na mtu anayecheza na miradi ya maendeleo sitaona shida kumchukulia hatua mtu yeyote atakayeharibu miradi ya maendeleo” amesema Msanga
Aidha Mkurugenzi huyo ametumia kikao hicho kuwapongeza Walimu ambao Shule zao zimefanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba wakiongozwa na Shule ya msingi Hungumalwa,Kakora na shule nyingine.
Pia ametumia kikao hicho kuwataka Walimu ambao shule zao zimekuwa za mwisho kwenye matokea ya darasa la saba kuongeza bidii ili matokea ya mwaka ujao wafanye vizuri zaidi. Shule hizo ni Kijida,ng’uliku,Dodoma,Mhalo na Shule nyingine.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.