Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe.Johari Samizi awataka Walimu Wakuu kuandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza wote wenye vigezo vya kuanza darasa la kwanza wanaopatikana katika maeneo yao ya kazi.
Ameyasema hayo tarehe 12 Jan, 2022 alipokua akifanya kikao na Walimu katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Ngudu. Mkuu huyo amesema kuwa walimu wanapaswa kuelewa kuwa Shule isopokua na wanafunzi walimu hawatakua na kazi ya kufanya hivyo wajitahidi kuwaandikisha wanafunzi hao ili kufikia tarehe 17/01/2022 wote wawepo shuleni na waanze masomo kama wanafunzi wa madarasa mengine.
"nendeni mkaandikishe watoto, watoto wasipokuja huna haja ya kuwa na shule na ninaamini kiwanda cha uzazi kiko vizuri kwahiyo watoto wapo naomba waandikishwe" alisema Samizi
Aidha Mkuu huyo amewakumbusha walimu majukumu yao "Tendeeni haki taaluma zenu, wajibikeni kwa Mwajili, wajibikeni kwa jamii" amesiwasisitiza Walimu kufanya majukumu yao kama inavyotakiwa"
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.