Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija akifungua semina za Walimu wanaotarajia kusimamia kazi mbalimbali za Elimu ikiwa ni pamoja na usimamizi wa mitihani Leo 16 Agosti,2023 amesisitiza uadilifu,uaminifu na umakini wakati wa shughuli za Kitaifa.
Mkuu huyo amewataka Walimu kusimamia kwa weledi na kutowatisha wanafunzi wakati wa mitihani " msiwatishe wanafunzi kwa maneno makali wakati mwingine vitisho vinasababisha mwanafunzi anasahau mambo yote aliyosoma" Ludigija
Katika semina hiyo ameshiriki Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Bi. Happiness Msanga ambaye amewataka Walimu kuwa makini na kuhakikisha hakuna kuruhusu wanafunzi kuangalizia
" ni marufuku wanafunzi kuangaliziana, Kwimba hatuna historia ya wanafunzi kuibia mitihani na hatutarajii kuwa na sifa hiyo, waacheni wanafunzi wavune walichokipanda" amesema Msanga
Naye Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza Mwalimu Mkwabi amewaelekeza Walimu kutimiza wajibu wao kama watakavyoelekezwa na wataalamu waliokuja kutoa mafunzo hayo, pia amesisitiza umakini na utulivu wakati wote wa mafunzo.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.