Akifungua mafunzo Ndug. Joshua Mgoli Afisa Utumishi(W) amesema MADENIMS (MADENI MANAGEMENT INFORMATION SYSTEM) ni mfumo wa kuingiza madeni yasiyo ya mshahara kwa kada ya walimu,mfumo huu unamuwezesha kila Mwalimu kuwa na akaunti ya kuingiza madeni kwa mfano madeni ya likizo,uhamisho na kazi nyingine hivyo mtumishi huyu anayaandika na kumtumia mkuu wake wa kazi kwa ajili ya utekelezaji.Afis Utumishi amewataka walimu waliopata mafunzo hayo kuwa mabalozi kwa walimu wengine ili kila Mwalimu ajue kuutumia mfumo huo ili uwasaidie kutuma madeni yao.
Mfumo huo umeonekana kuwa mzuri kwani unamuwezesha mtumishi kuangalia kama madai yake yameshafanyiwa kazi au la na hivyo mtumishi huyu anajua madai yake yanakwama ofisi gani hivyo kumpa urahisi wa kufatilia.
Wawezeshaji wa mafunzo hayo maafisa TEHAMA Ndug.William Kasuja na Emmanuel Magobo wamewasisitiza walimu hao kwenda kufanya kazi hiyo kulingana na mafunzo waliyoyapata pia wamewasisitiza walimu Wakuu kutochelewesha madai hayo pindi walimu wanapotuma madeni hayo Walimu wakuu wanapaswa kuyafanyia kazi na kisha kuyatuma kwa Afisa Elimu naye akishafanyia kazi anatuma sehemu husika kwaajili ya mwendelezo wa uhakiki na malipo.
Walimu hao wamesema mfumo huo ni mzuri kwani utawawezesha kuweka madai ya miaka iliyopita ili yaweze kufanyiwa kazi, vilevile wamesema mfumo huu Kama utafanya kazi Kama mafunzo yalivyoelekeza utasaidia madeni mengi kulipwa.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.