Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ludigija amewapongeza Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari kwa kuongeza ufaulu wa mitihani ya Taifa huku msiitizo ukiwa kwa walimu ambao hawajapata tuzo na zawadi kwenda kuongeza kasi ya ufundishaji ili waoengeze ufaulu katika Shule zao.
Pongezi hizo zimetolewa leo Agosti 9,2023 katika kikao cha tathimini ya Elimu kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ambapo Mkuu wa Shule ya Sekondari Sumve Bi. Clotilda Komenkesha ameibuka mshindi wa kwanza kwani Shule yake imekuwa ya nane Kitaifa katika Shule za wasichana katika matokeo ya kidato cha sita 2023.
Kupitia kikao hicho Mkuu wa Wilaya amewataka Walimu wote kwenda kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake ili Shule zote ziweze kuwa na ufaulu kama wa Sumve Sekondari au zaidi
" leo tumefurahi kuwapongeza wote ambao Shule zenu zimefanya vizuri lakini Kuna wachache ambao bado hawajafikia kiwango tunachokitaka, niwaelekeze wote kwenda kuongeza kasi ya ufundishaji ili tukikutana katika mwaka mwingine tuwe na Shule nyingi zilizoingia kumi bora Kitaifa" Ludigija
Aidha Mkuu huyo ameitumia nafasi hiyo kuwaelekeza Walimu wakuu na wakuu wa Shule kwenda kuweka mikakati itakayowezesha wanafunzi kupata chakula shuleni
" swala la chakula shuleni siyo jambo la hiari ni lazima kwahiyo mkaweke mikakati ya kukutana na wazazi mkubaliane namna bora ya upatikanaji wa chakula shuleni, haiwezekani mwanafunzi asome na njaa harafu utegemee afaulu mtihani, watoto wapate chakula shuleni" amesema Ludigija
Akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya Elimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi. Happiness Msanga amewapongeza Walimu wote walioongeza ufaulu katika masomo wanayofundisha. Pia amesema Halmashauri inaedelea na mikakati ya kuongeza ufaulu kwa kutoa hamasa na motisha kwa walimu wanaofanya vizuri.
Katika hafla hiyo zawadi za fedha,vyeti na ngao vimetolewa kwa walimu na Shule zilizofanya vizuri ambapo Shule za msingi zilizoonekana kuongoza katika matokeo ya darasa la nne na lasaba ni Mwamapalala na Ndagwasa na Shule za Sekondari zilizoongoza ni Sumve na Nyamilama.
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.