Wananchi wa kata ya Hungumalwa na Bungulwa wanufaika na Elimu ya Ugonjwa wa Fistula iliyotolewa tarehe 23 na 25,Februari 2021 kwenye maeneo ya minada ya Kata hizo na wawezeshaji kutoka Shirika la AMREF, Shirika la Maperece wakishirikiana na Wataalam mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba.
Wataalam hao wamesema Fistula ni hali ya kuwa na tundu lisilo la kawaida linalotokea kati ya kibofu cha mkojo au njia ya haja kubwa na uke au vyote kwa pamoja na kusababisha kutokwa mkojo au haja kubwa bila kujitambua.
Mwanamke mwenye fistula hutokwa na mkojo au haja kubwa au vyote kwa pamoja kupitia njia ya uzazi bila kujizuia, wamesema kuwa ugonjwa huo hutokana na mwanamke mjamzito anapotaka kujifungua kupata uchungu kwa mda mrefu na uzazi pingamizi.bila kupata huduma ya dharura ya uzazi.
Waliokuwa wahanga wa Fistula wametoa ushuda jinsi walivyo pata matibabu ya upasuaji katika Hospitali ya Bugando bure bila kulipia gharama yoyote 'ninaishukuru Serikali na Shirika la AMREF na MAPERECE kwa kunisaidia nimetibiwa ugonjwa uliokuwa umenisababishia kutengwa na mme wangu,na jamii kwa sababu nilikua na harufu mbaya sana ambayo nilidumu nayo kwa miaka mitano lakini sasa ninafuraha maana nimepona ninaishi kama wanawake wengine,amesema Suzana Yona
Bi. Suzana Yona, aliyekuwa mhanga wa Fistula
Aidha wataalamu hao wamewashauri wananchi kutowaficha wagonjwa wa fistula na wamesisitiza kuachana na imani potofu kuwa ugonjwa huo unatokana na imani za kishirikina na vitu vingine vinavyoendana na hivyo pia wamewasisitiza wanawake kuhudhuria kliniki pindi wanapokuwa wajawazito ili kujua maendeleo ya Mtoto anayekuwa tumboni , wameelekeza kuwa matibabu ta fistula yanafanyika kwenye hospitali ya Bugando tu kwa Mkoa wa Mwanza ila kwa Mikoa mingine ziko Hospitali zilizoteuliwa kwaajili ya matibabu hayo.
Mratibu wa Fistula (W) Bi. Salome Malale
Ngudu-Kwimba
Sanduku la Posta: P.O.BOX 88
Namba ya Simu: 0732 980528
Simu ya Kiganjani: 0732980528
Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.