• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Kwimba District Council
Kwimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Orodha ya viongozi
      • Orodha ya wenyeviti wa Halmashauri
      • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Orodha ya wakurugenzi
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Ufuatiliaji na Takwimu
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Usafi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Taka na Usafi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Utamaduni, Michezo na Sanaa
      • Kitengo cha Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • TEHAMA
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
      • Elimu
    • Elimu
    • Mkataba wa Hduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari
  • Machapisho
    • Fomu
  • Investment Opportunity
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika

WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

Posted on: March 21st, 2025


Afisa Elimu Sekondari Mwalimu Emmanuel Katemi amewataka wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyamilama kusoma kwa bidii  na kuhakikisha matokeo ya mitihani ya Taifa ufaulu unaongezeka zaidi.


Ameyasema hayo  leo Machi 21,2025 wakati akikagua utekelezaji wa maelekezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ya kuwapatia motisha wanafunzi wa Shule hiyo kwa kuwapikia chakula ( wali na nyama ya kuku)


" kikubwa kilichowaleta hapa ni elimu kwahiyo niwatake msome sana tena kwa bidii ili ufaulu uongezeke zaidi, mnajua hii shule ni miongoni mwa shule bora hapa Tanzania kwa Shule za Serikali  kwahiyo tunataka ufaulu uongezeke zaidi na mkifanya vizuri zaidi kwenye mitihani mtapata motisha nyingine nzuri zaidi" amesema Katemi


Aidha amewataka wanafunzi hao kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za shule hiyo ili kuwa na nidhamu nzuri, pia amewasisitiza  kuzingatia elimu maana ndiyo lengo kubwa lililowapeleka shuleni.


Naye Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Japhet  Sineno amemshukuru Mkurugenzi kwa kutoa motisha hiyo kwa wanafunzi kwani  itakuwa chachu kwao kupenda masomo zaidi na kuongeza juhudi ili mitihani ijayo wafanye vizuri zaidi.


Nao wanafunzi wameishukuru Serikali kwa kutoa motisha ya chakula hicho na wameomba motisha za namna hiyo ziendelee kuwa zinatolewa pindi wanapofanya vizuri katika mitihani,  wanafunzi hao wameahidi kufanya vizuri zaidi katika masomo yao.


Shule ya Sekondari  Nyamilama  imekuwa ikifanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya Taifa kwa zaidi ya miaka mitano  mfululizo jambo ambalo limewavutia wazazi wengi kupeleka wanafunzi  katika Shule hiyo ambayo kwa sasa  inawanafunzi wa kidato cha kwanza hadi  cha tano, na zaidi ya wanafunzi 1300 wanakaa bweni na hosteli.


DJI_0038.JPG

Matangazo

  • TANGAZO LA MNADA April 02, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO KWA WANAWAKE,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 07, 2024
  • TANGAZO LA MNADA WA MAGARI NA PIKIPIKI February 20, 2025
  • TAHADHARI YA KIPINDUPINDU September 12, 2024
  • Onyesha zote

Habari Mpya

  • WANAFUNZI WAHIMIZWA KUSOMA KWA BIDII

    March 21, 2025
  • MKUU WA WILAYA AHIMIZA USAWA WA KIJINSIA NA UWAJIBIKAJI

    March 06, 2025
  • WATENDAJI WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI ZA UKUSANYAJI MAPATO

    February 27, 2025
  • KWIMBA YATOA MILIONI 607 KWA VIKUNDI 37 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WALEMAVU

    February 21, 2025
  • Onyesha zote

Video

ZIARA YA MHESHIMIWA DC TARAFA YA MWAMASHIMBA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2016
  • Orodha ya watumishi wenye vyeti vya kugushi
  • Orodha ya Madaktari waliojariwa April 2017
  • Ajira mpya za walimu wa Hisabati na Sayansi 2016/2017
  • Matokeo ya Kumaliza Kidato cha Sita na Ualimu 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Tovuti ya ofisi ya Rais utumishi wa umma
  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza
  • Tovuti ya ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti ya Tume ya Maadili

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Mawasiliano

    Ngudu-Kwimba

    Sanduku la Posta: P.O.BOX 88

    Namba ya Simu: 0732 980528

    Simu ya Kiganjani: 0732980528

    Barua Pepe: ded@kwimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma zetu

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.